UMAJARIBIO KATIKA TAMTHILIYA MZALENDO KIMATHI.
UMAJARIBIO KATIKA TAMTHILIYA JINA LA TAMTHILIYA:MZALENDO KIMATHI. MWANDISHI:NGUNGI WA THIONG’O. PUBLISHER: East African Educational Publishers. Mwaka:1978. Utangulizi Tamthiliya ya Mzalendo Kimathi iliandikwa na Ngungi Wa Thiong’o mnamo mwaka 1976 na kilitolewa kwa Kiswahili na East African educational publisher mnamo mwaka 1978. Tamthiliya hii inahusu harakati za kudai uhuru nchini Kenya ambapo tunaona wananchi wa Kenya wanapigana vita vya Maumau dhidi ya ukoloni wa Mwingereza na katika harakati hizo wanakumbana na changamoto mbalimbali kama vile viongozi wao kufungwa jela na wakoloni. UMAJARIBIO Waandishi wa Tamthiliya ya Mzalendo Kimathi wametumia mbinu mbalimbali za fasihi simulizi katika kuwasilisha yale waliyokusudia katika jamii husika.Na mbinu hizo ni kama ifuatavyo;- 1.Matumizi ya Nyimbo. Katika onyesho la kwanza waandishi wameonyesha wananchi wakiimba nyimbo zinazodhirisha mapambano dhidi ya ukoloni au watu weupe waliokuwa w...